NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Uchunguzi wa endoscopy ya tumbo ni utaratibu wa uchunguzi unaotumiwa na daktari kukagua ndani ya koo, umio, tumbo, na utumbo wa juu.
Kuna kifaa ambacho hutumiwa kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Buriani Mwanahabari Shadrack Mitty

Sekta ya uanahabari imepata pigo mapema leo asubuhi baada ya kumpoteza mwanahabari Shadrack Mitty ambaye alikuwa akihudumu kama mwanahabari katika shirika la utangazaji la Standard Group.

Nuru AbdulAziz

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Shule Ya Msingi Ya Nyali Yafungwa

Shule ya msingi ya Nyali kaunti ya Mombasa ilifungwa leo kutokana na mzozo wa usimamizi wa shule hiyo.

Nuru AbdulAziz

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Baadhi Ya Shule Hazijafunguliwa

Katika kaunti ya Makueni baadhi ya shule hazijafunguliwa kufuatia mafuriko yaliyosababisha uharibifu wa barabara na miundomsingi ya shule.
Zaidi ya wanafunzi 70 wamekosa kurudi katika mojawapo ya shule.

Nuru AbdulAziz

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Muguka Wakurupuka Mombasa

Kulitokea fujo eneo la Bonje, Mombasa kufuatia mvutano baina ya maafisa wa kaunti na wafanyabishara wa zao la Muguka.
Askari wa kaunti walikuwa wanaitisha amri ya mahakama ya kubatilisha marufuku ya muguka.

Kevin Mutai

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

UDA Kumewaka Moto!

Sakaja amemtaja naibu rais Rigathi kama mtu ambaye amewahangaisha viongozi kwa muda wa miaka miwili.
Gavana wa Nyeri kwa upande wake anatishia kuanzisha mchakato wa kumng'atua kutoka chamani Cleophas Malala.

Chazima on X

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

NCIC Yatoa Makucha

Tume ya NCIC inasema kwamba inachunguza, matamshi ya viongozi waliofika katika mkutano wa Limuru 3.

Brian_Muchiri

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

NMG Yafaa Shule 4 Kisumu

Wakfu wa Nation Media Group umewasilisha msaada wa madaftari, sodo na vitabu kwa shule nne za kaunti ya Kisumu.

Nicholas Wambua

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Naboka Waomba Msamaha

Usimamizi wa chama cha ushirika cha matatu cha Naboka umejitokeza na kuwaomba msamaha Wakenya kuhusu ajali ya matatu iliyosababisha vifo vya watu 9.

Frederick Muitiriri

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Mananasi Ya Uchungu

Watu watatu wanauguza majeraha ya risasi kufuatia mzozo unaowakabili polisi na wakaazi wa Makenji kutokana na madai ya wizi wa mananasi katika shamba la Del Monte Kenya.

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Kenya Asumbukia Misri

Familia moja kutoka eneo la Ruiri, Meru inapitia wakati mgumu baada ya mwanao Lynette Makena kurushwa korokoroni nchini Misri baada ya cheti chake cha usafiri kumalizika muda wake wa matumizi.

Nicholas Wambua

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Bajeti Ya 2024/2025

Mapendekezo kadhaa ya ushuru mpya yaliyoko kwenye mswada wa fedha wa mwaka wa 2024 yanazidi kupokea pingamizi kutoka kwa washikadau kutoka sekta kadhaa nchini.

Nicholas Wambua

account_circle
NTV Kenya(@ntvkenya) 's Twitter Profile Photo

Marufuku Ya Muguka

Wakulima na wafanyibiashara wa Muguka wamewasilisha kesi mahakamani wakipinga marufuku dhidi ya Muguka katika kaunti za Pwani.

Frederick Muitiriri

account_circle
Simon Mogire Official(@simonmogir6691) 's Twitter Profile Photo

Ada Mpya Za Ntsa

NTSA yatoa mapendekezo ya ada mpya

Kubadilisha rangi kutoka Sh500 - Sh20,000 (3,900%)

Leseni ya wauzaji wapya kutoka Sh9,600 - Sh100,000 (942%)

Kubadilisha umiliki wa gari zaidi ya 1000cc ni Sh10,000 (502%)

#NTVJioni @FredMuitiriri
account_circle